Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ametoa onyo kwa viongozi wa ushirika wanaojihusisha na kusafilisha fedha
za serikali bila utaratibu huku akiwasisitiza kuwa wajitathimini kabla
ya maamuzi kutoka serikali kuu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Akizungumza
katika maadhimisho ya siku ya vyama vya ushirika duniani yaliyofanyika
jijini Mwanza Majaliwa amesema, viongozi ambao wanasafilisha fedha za
vyama vya ushirika kinyume na utaratibu na baadae kusema kuwa wamevamiwa
na kuporwa fedha hizo watawajibishwa kisheria.
"Wizi na ubadhirifu ulioshamiri unadhoofisha maendeleo ya
ushirika mjitathimini na kusababisha hasara kubwa na kuwa mzigo wa
serikali ili kulipa fedha hizo", amesema Waziri Mkuu Majaliwa
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa serikali itaangalia upya
mpangilio wa mnada wa kahawa mkoani Kilimanjaro na badala yake ufanyike
katika mikoa husika inayozalisha kahawa ili mkulima afike ,mwenyewe
kwenye mnada na kushuhudia bei halisi.
Waziri Majaliwa afunguka juu ya wanaojiteka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 07, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment