Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amelitaka Baraza jipya
la wadhamini la chama hicho kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kufanya
tathmini ya mara kwa mara ya mali za chama na jumuiya zake
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson
Msigwa imesema Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Julai 13, 2018 alipokutana
na wajumbe wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Magufuli amesema baraza hilo linapaswa kutekeleza
majukumu yake ipasavyo, ambayo ni kusimamia mali zote za chama na jumuiya zake,
kufanya tathmini ya mara kwa mara ya mali za CCM na jumuiya zake, kutoa ushauri
juu ya mabadiliko yoyote yanayohitajika katika umiliki wa mali
Mwenyekiti huyo amesema pamoja na kutekeleza majukumu
mengine ambayo yatakabidhiwa kwake na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa
Rais Magufuli amesisitiza hatarajii kuona dosari za
usimamizi wa mali za chama zikiendelea na amewataka wajumbe hao kuhakikisha CCM
inanufaika na mali zake na kuachana na utegemezi ambao umekuwa ukisababisha kuomba
misaada kutoka kwa watu.
Naye Mwenyekiti wa
baraza hilo Anna Abdallah amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwaamini na kuwateua
kuunda baraza hilo na ameahidi watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa
umakini na kwa maslahi ya CCM
“Mambo hayatakuwa kama walivyozoea huko nyuma kwamba kila
mtu anamiliki kipande chake cha mali za chama, hapana, mali zote za chama ni
mali ya Baraza la Wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi” amesema Anna
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema
baraza hilo la kwanza kuundwa baada ya kufanyika marekebisho ya katiba ya
chama, litasimamia mali za CCM pamoja na kusimamia utekelezaji wa mapendekezo
ya tume ya kufuatilia mali za chama ambayo yeye alikuwa mwenyekiti wake
Wajumbe wa baraza hilo ni; John Chiligati, Jaji mstaafu Mark
Bomani, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay, Pandu Ameir Kificho, Christopher
Gachuma, Dk Haruni Kondo na Hassan Omar Mzee
Rais Magufuli alitaka baraza la wadhamini la CCM kufanya tathmini ya mali
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 13, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 13, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment