Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemtaka Kamishna mpya wa Magereza
kuwatumia wafungwa katika ujenzi pamoja na uzalishaji kwa manufaa ya
jeshi hilo na taifa kwa ujumla.
Rais
Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla
ya kuwaapisha Balozi Joseph Edward Sokoine kuwa Naibu katibu Mkuu wa
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Martine Kasike ambao aliwateua
hivi karibuni.
Rais
Dkt. Magufuli amesema kuwa ni jambo la kushangaza kuona Jeshi hilo
linaomba msaada kwa serikali kwa ajili ya bajeti ya chakula na ujenzi wa
nyumba za watumishi wakati wana watu ambao wanaweza kuwatumia.
“Maana
ya kufungwa ni ukafanye kazi, maaskari magereza kazi yao ni kuwafanya
wafungwa wafanye kazi, ndio maana wengine wanahukumiwa na kuchapwa fimbo
ziwachangamshe wakafanye kazi”, amesema Rais Magufuli.
Ameongeza kuwa, “Ni
suala la aibu nchi kuendelea kulisha wafungwa, maeneo ya magereza ni
mengi mno ukienda kule Mbeya mashamba yanalimwa robo tu, kila mahali
kuna magereza na maeneo ya mashamba, lakini kila mwaka kunakuwa na
maombi ya bajeti kulisha wafungwa”.
Aidha
Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kumtaka Kamishna Jenerali wa Magereza
kuzuia wafungwa kuendelea kupata huduma ambazo ni kinyume cha sheria ya
magereza ikiwa ni pamoja na masiwasiliano ya simu.
“Kamishna sikupongezi, nakuhurumia sana”-JPM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 14, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment