Panya 4 wapelekwa Polisi kwa Kosa la kuharibu Pesa

Mfanyabiashara mmoja kutoka nchini Uganda amewapeleka panya watano katika Kituo cha Polisi cha Kotido Central katika tukio la kushangaza lililowaacha wanakijiji wenzake midomo wazi.

Peter Lojok Longolangiro aliwatuhumu ‘watuhumiwa ’ watano kwa kuharibu pesa zake alizokuwa ameweka ndani ya sanduku.

Mtandao wa Watchdog Uganda, umesema Longolangiro alidai kuwa panya hao walikula fedha za kenya  KSh 10,000 sawa na shilingi 227,404 za kitanzania, ambazo alifikisha mbele ya  kituo cha polisi kama ushahidi.
Panya 4 wapelekwa Polisi kwa Kosa la kuharibu Pesa Panya 4 wapelekwa Polisi kwa Kosa la kuharibu Pesa Reviewed by KUSAGANEWS on May 15, 2018 Rating: 5

No comments: