Mkazi wa kijiji cha Bubare kilichoko katika kata ya Kakungu
iliyoko wilayani Misenyi mkoani Kagera Josephat Joseph ameuwawa kwa
kupingwa risasi na askari waliokuwa kwenye harakati za kuokoa maisha yao
baada ya kuvamiwa na kundi la wafugaji waliotaka kuwanyanganya Ng’ombe
zaidi ya 300 waliokamatwa ndani ya katika kitalu namba 20 cha mwekezaji wa
kampuni ya Farmers Investment alichomilikishwa na kampuni ya ranchi ya
taifa (NARCO) eneo la Misenyi kwa ajili ya ufugaji wa kisasa na wa kibiashara
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na katika tukio
hilo mwananchi mwingine aliyetajwa kwa jina la Thomas Kasimbazi amejeruhiwa kwa
risasi na wananchi wamewajeruhi walinzi watatu wa kitalu namba 20, kufuatia
tukio hilo kamanda wa jeshi la Polisi wa mkoa wa Kagera Kamishina Msaidizi
Mwandamizi Augustine Ullomi amefika kwenye eneo la tukio na kuzungumza na
wananchi wa kitongoji cha Rwenkuba walioelezea juu ya tukio hilo ambapo
ameahidi kuwa serikali itachukulia hatua kali wale wote watakaobainika walihusika
na tukio hilo.
Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali Denis
Mwila kuwapa pole ndugu na jamaa wa mwananchi aliyepoteza maisha amewaondoa
wasiwasi wananchi kwa kuwaeleza kuwa serikali imeanza kutekeleza mikakati yake
ya kuimarisha masuala ya usalama kwenye maeneo ya mipaka ili iweze kudhibiti
vitendo vya uingizwaji holela wa mifugo toka nje vinavyofanywa na wananchi
wasio waaminifu ambavyo vinachangia migogoro, ametoa kauli hiyo baada ya
Charles Francis mwenyekiti wa tawi la Bubare la Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kuiomba serikali iwahakikishie usalama wananchi hao.
Mwanaume mmoja auawa baada ya kupigwa Risasi na Askari Mkoani Kagera
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment