Mkandarasi atazitapika hizo pesa” – Rais Magufuli

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuchukuliwa hatua kwa mkandarasi wa mradi wa maji katika kata ya Kidodo mkoani Mororgoro baada ya kushindwa kukamilisha mradi wa ujenzi huo licha ya serikali kutoa shilingi milioni 800.
Dkt. Magufuli amesema hayo leo Mei 04, 2018 katika ziara mkoani humo na kuongeza kwamba ni jambo lisilowezekana kwa nchi yenye vyanzo vingi vya maji kama Tanzania halafu wananchi wake wanakosa maji
“Ninafahamu kuna mradi wa shilingi milioni 800 ambapo kandarasi alipewa kazi na maji hayajafika kwa wananchi, ninachotaka kusema nitamtuma Waziri wa maji, atakuja aukague huu mradi kama mkandarasi amekula hizo hela atazitapika naomba mumfikishie huu ujumbe” amesema Rais Magufuli
Sambamba na hilo Rais Magufuli alimpigia simu katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo kwenda kushughulikia suala hilo mara moja kuanzia kesho kwa kumtafuta mkandarasi na kumrudisha katika mradi huo.
Rais Magufuli anafanya ziara mkoani Mororgoro akirejea jijini Dar es Salaam baada ya kutoka mkoani Iringa alipokua mgeni rasmi katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi.

Mkandarasi atazitapika hizo pesa” – Rais Magufuli Mkandarasi atazitapika hizo pesa” – Rais Magufuli Reviewed by KUSAGANEWS on May 04, 2018 Rating: 5

No comments: