Magufuli kuwakabidhi Kombe Simba


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya mabingwa Simba SC dhidi ya Kagera Sugar, Jumamosi hii ambapo atawakabidhi Simba taji lao. 

Hilo limebainishwa mchana huu na Rais wa shirikisho la soka nchini Wallace Karia, ambaye ameweka wazi kuwa wao kama shirikisho wameona ni vyema kumwalika Rais Magufuli kwenye tukio hilo maalum na muhimu kwenye mchezo wa soka nchini.

''TFF kwa kupitia Ofisi ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, tumetuma ombi kwa Mh. Rais Magufuli kwaajili ya kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo ili awakabidhi Simba taji la ubingwa na tunaamini atakubali'', amesema.

Magufuli kuwakabidhi Kombe Simba Magufuli kuwakabidhi Kombe Simba Reviewed by KUSAGANEWS on May 15, 2018 Rating: 5

No comments: