Magufuli atoa Bilioni 50

Jiji la Dar es salaam limepokea Shilingi Bilioni 50.09 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo standi kubwa ya kimataifa ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani.
Akiongea wakati wa kikao kazi cha kuanza ujenzi wa miundombinu hiyo kwa wilaya zote sita Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda amesema fedha hizo ni za serikali kutoka kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwaajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo lengo likiwa nikuziwezesha kuwa na miradi itakayozalisha fedha na kujitegemea ili kutoka kwenye utegemezi.
Aidha, Makonda amesema fedha hizo hazina riba ni mbadala wa fedha za maendeleo kutoka kwa wahisani ambao huwa wanatoa riba za kiwango kikubwa hali inayopelekea taifa kuwa na deni kubwa nje ya nchi.
Kuhusu ujenzi wa kituo kipya kikubwa cha uwekezaji cha Afrika Mashariki ambacho kinatarajia kujengwa ilipo stendi ya mabasi makubwa kwa sasa Ubungo Bus Terminal amesema wapo katika hatua nzuri kimchakato.
Miradi itakayotekelezwa na fedha hizo ni Kituo cha kimataifa cha mabasi makubwa ya abiria ya ndani na nje ya nchi kitakachojengwa Mbezi Luis, soko kubwa la Kisasa eneo la Kisutu,machinjio ya kisasa Vingunguti,madaraja,barabara na hospitali.
Magufuli atoa Bilioni 50 Magufuli atoa Bilioni 50 Reviewed by KUSAGANEWS on May 10, 2018 Rating: 5

No comments: