Kombe la Simba larudishwa nyuma


Mchezo namba 226 wa Ligi kuu Tanzania Bara kati ya mabingwa wa ligi Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC ya Morogoro uliopangwa kuchezwa Mei 20, 2018 kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam umerudishwa nyuma na hatimaye kuchezwa Mei 19 mwaka huu majira ya saa 8 mchana.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura na kusema sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuongeza ufanisi katika hafla ya kukabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.

Simba itarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumamosi huku ikiwa na alama 68 baada ya mechi 68 huku Kagera Sugar ikiwa na alama 31 baada ya mechi 28 ikiwa katika nafasi ya 10 kati ya timu 16 zilizoshiriki ligi kuu msimu wa 2017/18.


Kombe la Simba larudishwa nyuma Kombe la Simba larudishwa nyuma Reviewed by KUSAGANEWS on May 15, 2018 Rating: 5

No comments: