Mbunge wa Chalinze, Mh. Ridhiwani
Kikwete amefunguka na kuweka wazi kuwa klabu Yanga inahitaji mfumo sahihi wa
uendeshaji wa mpira ambao utaweza kuwasaidia katika kukabiliana na changamoto
mbalimbali hasa za kukosekana kwa pesa ili waweze kufanya vizuri katika michezo
yao inayowakabiri.
Mhe. Ridhiwani ametoa kauli hiyo
kupitia moja ya mijadala ambayo ilikuwa inaendeshwa katika mtandao wa kijamii
twitter ukiwa na lengo la kutoa hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa wanajangwani
kujitokeza kwa wingi viwanjani ili waweze kujikusanyia mapato mengi
yatakayotokana na watu kuingia uwanjani na sio kusubiri kuichangia muda ambao
itakuwa imekwama kabisa.
"Yanga wanaitaji mfumo sahihi
wa uendeshaji wa mpira utaolezea jinsi ya kukabiliana na changamoto ya
kukosekana kwa pesa, kuacha kutegemea mtu, kutafuta vyanzo vya mapato vya
uhakika, kulipa pesa kwa wakati na mengineyo yanayohusu mfumo wa mafanikio
katika soka", ameandika
Ridhiwani
Licha ya Ridhiwani kutoa ushauri kwa
Yanga lakini mmoja ya wadau waliokuwa wanachangia mjadala huo amesema "ukianza
kuusaka huo mfumo bora wa kuindesha Yanga ndio wanatokea kina Akilimali
wanaleta fujo, timu ikipoteza 'direction' nao wanakaaa kimya, 'so long as' kuna
watu wana maslahi binafsi ndani ya Yanga, mabadiliko ni ngumu sana
kuyapata".
Kikwete aishauri Yanga SC
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment