Ajali za barabarani zaua watu 15 nchini Kenya


Watu wasiopungua 15 wameuawa na wengine zaidi ya kumi wakijeruhiwa katika ajali mbili zilizotokea nchini Kenya mapema jumapili hii.

Abiria wanane wameuawa na wengine sita wakijeruhiwa katika ajali kati ya Daladala iliyogongana na lori kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi eneo la Mwambi mashariki mwa Kenya.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa kaunti ya Machakos Joseph Tenai, amesema dereva wa matatu alishindwa kudhibiti gari na kuliparamia lori, jambo lililopelekea watu sita kufariki papo hapo na wengine wawili walikufa hospitali wakati wakipata matibabu.

Katika ajali nyingine, watu saba wamefariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Probox kusombwa na mafuriko kwenye kata ya Githabai iliyoko katika jimbo la Kinangop kaskazini magharibi mwa Kenya kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo ya nchi hiyo.

Mkuu wa Polisi nchini Kenya IGP Joseph Boinnet amewasihi watumiaji wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari katika kipindi hiki ambacho barabara nyingi hazipitiki kutokana na hali mbaya ya hewa.

Ajali za barabarani zaua watu 15 nchini Kenya Ajali za barabarani zaua watu 15 nchini Kenya Reviewed by KUSAGANEWS on April 22, 2018 Rating: 5

No comments: