Watoto wawili wafariki wakichota maji


Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye dimbwi wakati wakichota maji kwa matumizi ya nyumbani

Watoto hao Lucia Ziada (10) na Joshua Ziada (6) ambao ni watoto wa Kassim Ziada mkazi wa Rwangasa wilayani Geita mkoani hapa
Mkuu wa wilaya ya Geita, Herman Kapufi amethibitisha kutokea vifo hivyo na kusema vimetokea jana Aprili 23 majira ya alasiri na kwamba mtoto Joshua ndio alianza kuzama na Lucia aliingia kumuokoa, naye akazama

Amesema marehemu hao waliambatana na mdogo wao, Justin Ziada (3) ambaye naye alizama lakini aliokolewa na hali yake inaendelea vizuri

Amesema dimbwi hilo lilichimbwa wakati wa ujenzi wa barabara ya Rwamgasa kwenda Katoro ambayo bado haijakamilika na kutokana na mvua zinazoendelea mawasiliano ya barabara hiyo yamekatika.

Watoto wawili wafariki wakichota maji Watoto wawili wafariki wakichota maji Reviewed by KUSAGANEWS on April 24, 2018 Rating: 5

No comments: