Shule ya msingi
Mnyonga ambayo ni ya mchanganyiko pamoja wanafunzi wenye Ulemavu
iliyoko Peramiho mkoani Ruvuma inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo upungufu wa madarasa ambapo kati ya madarasa kumi na
mbili yanayotakiwa kwasasa ina madarasa manne tu.
Changamoto hizo zimeelezwa na
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo Mwalimu Monica Kasia ambapo
amesema kuwa shule hiyo pia ina upungufu wa Madawati wanafunzi wanakaa chini,
ukosefu wa Bwalo la kulia hivyo wanafunzi hula wakiwa wameketi kwenye Nyasi
na pia haina Jiko na hivyo Mpishi hupika akainyeshewa na mvua.
|
|
Kutokana na changamoto hiyo
jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Songea vijijini imetoa misaada
mbalimbali kupunguza baadhi yachangamoto zinazoikabili shule hiyo
|
SHULE YA MSINGI MNYONGA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MADAWATI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment