Muigizaji na mchekeshaji wa siku
nyingi, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto, amelazwa tena katika Hospitali ya Tumaini
jijini Dar es Salaam, baada ya kuzidiwa.
Mke wa mwigizaji huyo, Aisha
Yusufu, ameiambia MCL Digital leo Aprili 23 kwamba mume wake walimpeleka
hospitalini hapo leo saa 7:00 mchana.
Aisha amesema kidonda alichofanyiwa
upasuaji kimeleta shida, hivyo kumpeleka kwa ajili ya uangalizi zaidi.
Majuto alilazwa hospitalini hapo
Januari mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa tezi dume.
Mzee Majuto azidiwa, arudishwa hospitali
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment