Muigizaji Salman Khan Afungwa miaka 5 jela kwa Ujangili

Muigizaji marufu wa filamu wa India Salman Khan amehukumiwa miaka mitano jela, kwa kosa la ujangili alilolifanya mwaka 1998.
Hukumu hiyo imetolewa leo na mahakama ya India baada ya kumkuta na hatia, huku waigizaji wenzake Saif Ali Khan, Tabu, Sonali Bendre na Neelam Kothari wakiachiwa huru kutokana na kutokutwa na hatia.
Salman Khan alishtakiwa kwa kosa la ujangili la kuua wanyama wawili wanaojulikana kama 'blackbucks' ambao ni jamii ya swala wa kipekee walioko nchini India, na serikali ya nchi hiyo inawatunza kwa uangalizi mkubwa.
Salman Khan alifanya tukio hilo katika kijiji cha Kankani ambako alikuwa akiigiza filamu yake ya Hum Saath Saath Hain , akiwa na waigizaji wenzake.

Muigizaji Salman Khan Afungwa miaka 5 jela kwa Ujangili Muigizaji Salman Khan Afungwa miaka 5 jela kwa Ujangili Reviewed by KUSAGANEWS on April 05, 2018 Rating: 5

No comments: