JOHN HECHE ACHEFUKWA


Mbunge wa Tarime (Chadema), John Heche amesema nchi nyingi duniani zimeingia kwenye machafuko kutokana na viongozi kupuuza baadhi ya mambo

Heche ameyasema hayo leo Aprili 12, bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais na akaongeza kwa kutoa mfano kuwa Rwanda iliingia kwenye machafuko baada ya watu kuamua kulipiza kisasi kutokana na kupuuzwa na kuonewa

“Leo hapa Tanzania kule Musoma, mwaka 2010, yaliwahi kutokea mauaji ya kulipiza kisasi, watu wa familia moja waliuawa kwa sababu ya visasi. Walikufa mpaka mbwa, paka na kuku. Leo nchi hii, watu wanapigwa, kwa sababu wengine wanafikiri wapo salama na wapo kwenye madaraka, wanaona ni sawa hawa kufanyiwa hivyo,” amesema

Heche amesema anajua kuwa ni miongoni mwa watu ambao wapo kwenye orodha ya kuumizwa na tayari ameshaiambia familia yake
“Katibu wetu wa kata ameuawa, watu mnaona ni sawa, Tundu Lissu amepigwa risasi, mnaona ni sawa.” Amesema

JOHN HECHE ACHEFUKWA JOHN HECHE ACHEFUKWA Reviewed by KUSAGANEWS on April 12, 2018 Rating: 5

No comments: