Wizara yaeleza kuhusu ndege ya Urusi iliyopata ajali Syria


Wizara ya ulinzi ya Urusi imetoa maelezo kamili kuhusu ndege iliyoanguka Syria na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30.

Kwa mujibu wa habari,ndege hiyo aina ya Antonov-26 haikushambuliwa kwa namna yoyote ile na kwamba uchunguzi kuhusu ajali  hiyo umeanzishwa.

Imeripotiwa kuwa watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo walipoteza maisha na kwamba wote walikuwa ni askari wa jeshi la Urusi.

Hapo awali ilitangazwa kuwa abiria 26 na wafanyakazi 6 walipoteza maisha lakini idadi kamili ni abiria 33 na wafanyakazi sita ndio waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Wizara yaeleza kuhusu ndege ya Urusi iliyopata ajali Syria Wizara yaeleza kuhusu ndege ya Urusi iliyopata ajali Syria Reviewed by KUSAGANEWS on March 07, 2018 Rating: 5

No comments: