Wananchi wa kijiji cha Majengo kata ya Njengwa halmashauri ya mji wa Nanyamba mkoani Mtwara wameamua kuunganisha nguvu zao na kujenga kituo cha afya, baada ya kuchoshwa na adha wanayoipata ya kufuata huduma za afya katika kijiji jirani cha Njengwa.
Wakizungumza wakati wa ujenzi huo, wananchi hao wamesema kukamilika kwa kituo hicho kutawasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa wenzao wa kijiji cha Njengwa ambako ndiko wanakopata huduma kwa sasa.
Kwa upande wake, mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota, amesema sambamba na jitihada hizo za wananchi, serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1.4 kwa ujenzi wa vituo vitatu vya afya.

Wananchi wachoka na manyanyaso
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 05, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment