Msafara wa Polepole wapata ajali kigoma

Msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Ndg Humphrey Polepole umepata ajali katika eneo la kijiji cha Nyamidaho, Kata ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kulia.

Aidha amesema kuwa waliojeruhiwa ni pamoja na Katibu wa CCM mkoa Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa UVCCM Sylivia Sigura pamoja na Katibu Mwenezi, Feruz ambao wamekimbizwa katika hosiptali ya wilaya ya Kibondo kwa matibabu.

Mwenezi ndg. Poplepole amewasili leo mkoani Kigoma na kupokelewa wilayani Uvinza akitokea mkoani Tabora ambapo atakuwa kigoma kwa takribani siku tatu.
Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota V8 yenye namba T150
Msafara wa Polepole wapata ajali kigoma Msafara wa Polepole wapata ajali kigoma Reviewed by KUSAGANEWS on March 05, 2018 Rating: 5

No comments: