Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani
Kihamia na Mkurugenzi wa shule ya msingi Upendo Friends Bi Isabela Mwampamba wakiwa
katika picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu wa macho leo wakati
wakikiabidhiwa vyoo vya matundundu sita shule ya msingi Themi jiji la Arusha
Walimu wakiwa na watoto wa shule ya msingi
Themi wenye ulemavu wa macho wakiwa wamekaa kwenye hafla ya kukabidhiwa
vyoo na mkurugenzi wa Shule ya Upendo Friends
|
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani
Kihamia na Mkurugenzi wa Shule ya Upendo Friends leo katika tukio la kukabidhi
vyoo vya wanafunzi wenye ulemavu wa kuona
|
Wanafunzi wa Shule ya msingi Themi jiji la
Arusha
|
Wanafunzi wenye ulemavu wa kuona wakiimba
wimbo katika hafla ya leo katika shule ya msingi Themi
|
Mkurugenzi wa Shule ya msingi Upendo Friends
Bi Isabela Mwampamba akisema jambo katika hafla ya leo
|
Mkurugenzi wa Shule ya Upendo Friends Bi Isabela
Mwampamba amekabidhi vyoo 6 vya kisasa vyenye dhamani ya Shilingi milioni 22.5
kwa ajili wanafunzi wenye ulemavu wa kuona katika shule ya msingi Themi iliyoko
katika jiji la Arusha.
Akimkabidhi mkurugenzi wa jiji la Arusha Vyoo hivyo Bi
Isabela amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo CRDB
BANK,Bulk Distributor na wengineo wamefanya hivyo kwa lengo la kuwasaidia
wanafunzi hao ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya sehemu kwa ajili ya
Kujisitiri.
Amewahamasisha wadau wengine mbalimbali kuguswa na
kujitoa kuwasaidia wenye uhitaji maalumu;kwa kuwa yeye pamoja na wenzake
wamekuwa mfano.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Juma Kihamia
ameshukuru kwa msaada huo, na kusema kwamba Mama Isabela anatekeleza ilani ya
Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuwa ilani ndiyo inayoongoza shughuli za serikali
na kuwenye ilani imeeleza kwamba serikali itashirikiana na wadau mbalimbali
kutatua changamoto za kijamii.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Zebedayo Moleli amesema vyoo
hivyo ni msaada mkubwa kwa watoto hao kwani vitawasaidia kuepuka magonjwa ya
mlipuko kutokana na changamoto inayowakabili.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Akabidhiwa Vyoo kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kuona
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment