MAHAKAMA YAWAACHIA HURU WATUHUMIWA MAKOSA YA MTANDAONI, POLISI YAWADAKA TENA


Mhakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Machi 12, 2018 imezifuta kesi mbili za makosa ya mtandaoni, namba 325/17 na 333/17 zilizokuwa zikiwakabili Obadiah Frank Kiko Mkazi wa Chato mkoani Geita na Hafidhi Khamis kutoka Zanzibar baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kukamilisha ushahidi.
Uamuzi huo umekuja baada ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri kutoa angalizo kwa upande wa jamhuri kufuatia kushindwa kuwasilisha ushahidi wao kwa zaidi ya mara tatu mahakani hapo.
Wakili upande wa utetezi, Wakili Msomi Alex Massaba amesema baada ya watuhumiwa hao kuachiwa huru na mahakama, walikamatwa tena na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Amesema wanapanga kwenda Mahakama Kuu kuomba tafsiri ya kifungu namba 225 (5) cha Sheraia ya Makosa ya Mtandaoni kwa madai kuwa kinatumiwa vibaya na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

MAHAKAMA YAWAACHIA HURU WATUHUMIWA MAKOSA YA MTANDAONI, POLISI YAWADAKA TENA MAHAKAMA YAWAACHIA HURU WATUHUMIWA MAKOSA YA MTANDAONI, POLISI YAWADAKA TENA Reviewed by KUSAGANEWS on March 12, 2018 Rating: 5

No comments: