Mabweni ya Shule ya Korogwe Girls yaungua Moto

MABWENI mawili katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

Moto huo ulianza kuunguza mabweni hayo saa tatu usiku na chanzo chake hakijajulikana.Hata hivyo inadaiwa huenda chanzo kikawa ni umeme ingawa bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa moto huo.

Akizungumza leo, kwa njia ya simu na kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ,Edward Bukombe amesema atatoa taarifa rasmi na kwa sasa yupo eneo la tukio hilo."Nipo eneo la tukio na baada ya hapo nitakupa taarifa rasmi."

Mabweni ya Shule ya Korogwe Girls yaungua Moto Mabweni ya Shule ya Korogwe Girls yaungua Moto Reviewed by KUSAGANEWS on March 05, 2018 Rating: 5

No comments: