LHRC kwa NEC kufanyia kazi changamoto walizotaja

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufanyia kazi changamoto zilizoibuliwa na wadau wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge Kinondoni na Siha bila kujali udhaifu katika uwasilishaji wa changamoto hizo

Kituo hicho kimedai kuwa kuibuliwa kwa changamoto hizo kunalenga kujenga jamii yenye haki na usawa.

yameelezwa leo Jumatano Machi 7, 2018 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Naemy Sillayo alipokuwa akijibu hoja zilizotolewa na NEC wiki iliyopita kutokana na tamko lililotolewa na asasi za kiraia

Sillayo amesema tamko hilo halikutolewa na LHRC bali lilitolewa na umoja wa asasi za kiraia ambao kituo hicho ni mwanachama.

Sillayo amesema LHRC inakubaliana na hoja iliyotolewa na azaki ya kutaka NEC kuboresha kanuni za usimamizi wa uchaguzi na kutovibana vyombo vya habari

“Hilo litasaidia kutoweka mipaka kwa vyombo vya habari wakati wa kutimiza jukumu la kutoa taarifa kwa umma,"amesema.
LHRC kwa NEC kufanyia kazi changamoto walizotaja LHRC kwa  NEC kufanyia kazi changamoto walizotaja Reviewed by KUSAGANEWS on March 07, 2018 Rating: 5

No comments: