Mkurugenzi wa halmashauri ya
Arusha vijijini Dokta Charles Mahera amewataka wanawake kujikomboa kwa
kuwa mstari w mbele katika kutokomeza mila potofu zinazowanyima kushiriki
katika mipango ya maendeleo pamoja na kupiga vita mimba za utotoni.
Dokta Mahera amesema wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani katika halmashauri
hiyo ambapo katika kuhakikisha halmashauri hiyo inakuwa sehemu ya kuwasaidia
wanawake kuondokana na Changamoto hiyo ameiagiza Idara ya ustawi wa jamii
kabla ya kufika June mwaka huu kuhakikisha kamati zinazopinga ukatili kwa
wanawake na watoto zinaundwa katika kata zote 27 za halmashauri hiyo.
Lengai Ole Sabaya diwani wa
kata ya Sambasha amesema kuwa pamoja na changamoto nyingi wanazokumbana
nazo wanawake bado dunia inajua umuhimu wao hasa katika ustawi wa
familia hivyo wa kama Viongozi wananafasi kubwa ya kutatua changamoto hizo
hasa katika suala la ukeketaji na unyanyasaji.
Hindu Ally Mbwega Mkurugenzi
wa kituo cha maendeleo ya wanawake,watoto na Vijana amesema kuwa unyanyasaji wa
wanawake na watoto umekuwa ni mwingi kupita kiasi kutokakana na mambo mengi
kufanyika kichinichini hasa maeneo ya pembezoni ikiwa ni pamoja na haki
kupotelea mahakamani.
Dokta Mahera awataka wanawake Kujikomboa kwa kuwa Mbele.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment