DC Msafiri na Mbunge Dk Nagu waondoa Tofauti zao


Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Sarah Msafiri na mbunge wa Hanang, Dk Mary Nagu wamemaliza tofauti zao baada ya wiki iliyopita mkuu wa wilaya kuagiza mbunge ahojiwe polisi kwa kuchonganisha Serikali na wananchi.

Mwishoni mwa wiki wawili hao walikutanishwa katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti baada ya kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa kwa ajili ya kumaliza tofauti zao.

Sarah akizungumza akiwa na Dk Nagu wakimsubiri Mnyeti azungumze na kamati ya siasa ya CCM wilayani humo amesema hawana tofauti yoyote.

"Mimi na mama yangu Dk Nagu hatuna tatizo lolote ndiyo sababu mnatuona hapa tupo pamoja kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Hanang," amesema Sarah.


DC Msafiri na Mbunge Dk Nagu waondoa Tofauti zao DC Msafiri na Mbunge Dk Nagu waondoa Tofauti zao Reviewed by KUSAGANEWS on March 12, 2018 Rating: 5

No comments: