Bob Junior aingia matatani


Mmiliki wa Sharobaro records na staa mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Bob Juniour ambaye kumekuwa na tetesi kuwa anatafutwa na polisi kwa kosa la kumpiga aliyekuwa mpenzi wake na muigizaji wa Bongo movie Sabrina au maarufu kama Sabby Angel.

Sabrina amefanya interview na mtangazaji Soudy Brown wa Clouds Fm katika kipindi  cha U Heard na amesema kuwa Bob Junior amempiga kutokana na yeye kumwambia waachane kwasababu haoni maisha yakiendelea kati yao na amekuwa akilazimisha mapenzi.

Sabrina amesema…Kweli kuna matatizo yametokea, unajua mtu huwezi kulazimisha mapenzi nikikwambia it’s over its over lakini yeye anaforce mapenzi, ananipiga mambo ya zamani kwanza siku hizi mwanamke hapigwi unanipiga umenitolea mahari?

“Nimeona hana future nikaamua kumuacha lakini mtu hataki kuelewa anakuja ananipiga mi naona kama naonewa”

Sabrina na Bob Junior inasemekana kuwa wamekuwa katika uhusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya miaka nane hata kabla ya Bob Junior kufunga ndoa na aliyekuwa mke wake Halima.

Bob Junior aingia matatani Bob Junior aingia matatani Reviewed by KUSAGANEWS on March 21, 2018 Rating: 5

No comments: