Chama cha Wauguzi nchini kimetoa onyo kali kutokana na kitendo cha kushambuiliwa alichofanyiwa muuguzi wa hospitali ya Bugando na kuiomba serikali kuchukua hatua dhidi ya matukio hayo.
Akizungumza na vyombo vya habari mkoani Mwanza Makamu wa Rais chama cha Wauguzi nchini Ibrahim Mgoo amesema wao kama chama cha wauguzi wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kushambuliwa kwa muuguzi aliyekuwa akimuhudumia mgonjwa aliyekuwa amelazwa katika hospital hiyo huku akilaani vikali tukio hilo.
Ikiwa ni takribani siku 12 zimepita tangu kutokea tukio la kushambuliwa kwa muuguzi huyo tukio hilo limeendelea kulaaniwa vikali na viongozi wa chama cha wauguzi hao, ambao wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo la udhalilishaji wa utu na taaluma ili kutoathiri utendaji kwa wauguzi wengine nchini.
Inadaiwa kwamba siku moja kabla ya mauti kumfika mgonjwa aliyekuwa anahudumiwa na muuguzi huyo, ndugu zake walikuwa wamelazimisha kubakia katika chumba cha uangalizi maalum, jambo ambalo halikukubaliwa na muuguzi huyo na siku iliyofuata walipoarifiwa kuwa ndugu yao amefariki, ndipo inadaiwa waliamua kumshambulia na kumjeruhi muuguzi huyo wakati akitoa huduma kwa wagonjwa wengine

Wauguzi wakasirishwa na Mwenzao Kushambuliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment