Treni mbili, moja ya mizigo na nyingine ya abiria leo
zimegongana Kaskazini mwa Misri na kusababisha vifo vya watu 15.
Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Misri, mbali na vifo hivyo,
ajali hiyo iliyoweka historia ya ajali kwa njia ya reli katika eneo hilo la
jimbo la Behaira ilisababisha watu wengine kumi na tano kujeruhiwa vibaya.
Kipande cha video inayoonesha tukio hilo kilichorushwa kwenye
televisheni ya taifa kimeonesha wananchi wakisaidiana na kitengo cha wizara ya
afya kuwaondoa majeruhi na kuwaweka kwenye magari ya wagonjwa (ambulances).
Afisa wa Wizara ya afya, Alaa Othman aliiambia televisheni ya
taifa kuwa majeruhi walikimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu na kwamba
miili yote ya marehemu iliondolewa kwenye eneo la tukio.
Sababu ya ajali hiyo bado haijafahamika. Tukio hilo limetokea
ikiwa ni miezi saba imepita tangu watu 41 wapoteze maisha baada ya treni mbili
kugongana katika jiji la Alexandria.
WATU 15 WAFARIKI KATIKA AJALI YA TRENI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment