Jaji Mkuu wa Tanzania,
Prof. Ibrahim Hamis Juma ameishauri Serikali kuishirikisha Mahakama kwenye
mipango yake ya uanzishaji wa maeneo mapya ya kiutawala ili kupunguza
changamoto za upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara yake
mjini Kigoma, Jaji Mkuu amesema mipango ya Serikali ya uanzishwaji wa Wilaya au
Mikoa uzingatie pia uanzishwaji wa Mahakama na kwamba, Mikoa na Wilaya mpya
ndizo zenye ukosefu wa Mahakama hali inayowafanya wananchi kufuata mbali huduma
za Kimahakama.
Akitolea mfano wa Wilaya ya Uyui,
Mkoani Tabora, Jaji Mkuu amesema, kutokana na Wilaya hiyo kuzunguka Mkoa,
wananchi wake hulazimika kufuata huduma za Mahakama Kuu zilizopo umbali wa
zaidi ya kilometa 377.
Amefafanua kwamba, kupitia Mpango wa
Maboresho Mahakama itaanzisha Mahakama zinazotembea yaani Mobile Courts, kwenye
maeneo yote yenye changamoto kama hizo kabla ya kujenga Mahakama kwa kuwa
changamoto ya upatikanaji wa huduma za Kimahakama bado ni kubwa nchini.
MAHAKAMAYAJA NA MPANGO HUU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment