Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mrisho Gambo amewasimamisha kazi Afisa Mifugo wa Wilaya ya Karatu, Mtendaji wa
Kijiji pamoja na Afisa Mifugo wa kijiji, kutokana na uzembe wa kiutendaji,
kwenye zoezi la kupiga chapa mifugo.
Mrisho Gambo ametoa agizo hilo baada ya kugundua kuwa watendaji hao wa serikali walikuwa hajatekeleza agizo la serikali la kupiga chapa mifugo, huku akiamuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kumuandikia barua ya Onyo Mkurugenzi wa Karatu.
“Nataka nikutaarifu kuwa kuanzia sasa namsimamisha kazi Afisa Mifugo wa wilaya, Mtendaji wa Kijiji hiki pamoja na Afisa mifugo anayehusika na kijiji hiki, lakini pia Katibu Tawala Mkoa amuandikie barua ya onyo Mkurugenzi wa Halmshauri ya Karatu, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashuri ya Karatu kwa hili”, amesema Mrisho Gambo.
Zoezi la kupiga chapa mifugo ni agizo kutoka serikalini ambapo mifugo yote nchini inatakiwa kupigwa chapa, ili kuweza kutambua takwimu zake na kuepusha migogoro.

RC GAMBO ATUMBUA AFISA MIFUGO NA MTENDAJI WA KIJIJI WILAYANI KARATU.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment