Nabii Tito afikishwa mahakamani

Tito Onesmo Machibya anayejulikana kama 'Nabii' Tito (44) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nong'ona Manispaa ya Dodoma leo Januari 29, 2018 amepandishwa mahakamani katika mahakama ya wilaya kwa shtaka la kutaka kujiua.

Nabii Tito amepandishwa kizimbani leo akidaiwa kutaka kujiua mwishoni mwa wiki jana ambapo alijichana chana na wembe katika baadhi ya maeneo ya mwili wake wakati Jeshi la Polisi likifanya uchunguzi nyumbani kwake.

Januari 23, 2018 Nabii Titoo alikamatwa na jeshi la polisi akituhumiwa kufanya uchochezi na baadaye alipelekwa kupimwa akili katika hospitali ya wagonjwa wa akili (Mirembe) na kufahamika kuwa mtu huyo alikuwa na matatizo ya akili, hivyo jeshi la polisi liliendelea kumshikilia kwa ajili ya usalama wake na siku jeshi hilo lilipokwenda kufanya uchunguzi nyumbani kwake ndipo alifanya jaribio la kutaka kujiua.
Nabii Tito afikishwa mahakamani Nabii Tito afikishwa mahakamani Reviewed by KUSAGANEWS on January 29, 2018 Rating: 5

No comments: