Madiwani watatu (CHADEMA)katika halmashauri ya Siha
mkoani Kilimanjaro wanatarajiwa kuburuzwa mahakamani kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwatetea
watumishi wa halmashauri hiyo waliofanya ubadhirifu wa zaidi ya shilingi
milioni 60 na kupokea rushwa katika geti ya kupitishia mazao.
Madiwani wa kata hizo (Kirua) Bwana Robert Mrisho Kata
ya (Ivaeni) Bwana Eliya Kiwia na diwani wa viti maalum Witnes Riwa wanatuhumiwa
kuchukua rushwa kwa watumishi walioibia halmashauri fedha ili kuwatetea katika
baraza la madiwani.
Taarifa zinasema kuwa Diwani wa kata ya Kirua Robert
mrisho amekuwa akijihusisha na rushwa katika shamba la shule kwa kumtetea ili
lirudi mikononi mwake.
Kusaga news ilizungumza na mmoja ya madiwani hao
wanaotuhumiwa wa kata Kirua Robert Mrisho amesema kuwa tuhuma hizo siyo za
kweli ni uzushi wa watu wachache wanaotaka kuharibu halmashauri hiyo.
Robert amesema hawakujihusisha na lolote na Mamlaka ya
Takukuru haijawahi kumuita wala kumchunguza kuhusu tuhuma hizo zinazodaiwa ni
za rushwa.
“Kimsingi maamuzi ya baraza la madiwani hayaongozwi na
diwani wa kata ya kirua au diwani wa viti maalum bali ni maamuzi baraza zima na
baraza la siha limebalance tulifanya
maamuzi ya pamoja sasa hakuna habari ya diwani yoyote anayejusika na kimsingi
kuna watumishi walikiri moja kwa moja kwamba walihusika na siyo milioni 60 bali
ni milioni 47 ambazo zilipotea kwenye mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya
Leseni”Alisema diwani Robert
MADIWANI 3 HALMASHAURI YA SIHA KUBURUZWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment