Lowasa" Nimesikitishwa sana na Maneno ya Kigwangala"

"Nimesikia taarifa za Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla akitaja jina la Lowassa kama mmoja ya watu eti walioshiriki kupora ardhi  Arusha.

Nimesikitishwa sana na matamshi hayo kutoka kwa waziri ambaye kwa mtu mwenye wadhifa wake kutoa kauli zisizo na msingi wowote na kulaghai Umma.

Nimemfahamu Mhe Kigwangalla kwa miaka mingi, tangu wakati anavurugana na mbunge mwenzake wa Nzega na rafiki yangu Mhe Hussein Bashe kule Nzega.

Kwa maoni na mawazo yangu nimekuwa nikiamini kwamba Kigwangalla atakuwa mtu aliyebadilika na kujifunza kutoka na makosa yake ya nyuma.

Kauli yake ya leo ni ushahidi kwamba bado ana matatizo yale yale ya kukurupuka.

Ni wazi hata baada ya mambo mengi kubadilika na pengine nyakati za kuchafua watu kukoma, ndugu huyu bado anaishi nyakati zile zile.

Ni wazi Kigwangalla anatumia vibaya dhamana aliyopewa na Rais Magufuli , kwa mambo ambayo Wizara ya Ardhi ina Wataalamu na uwezo wa kuchukua hatua stahiki kwenye mgogoro wowote.

Nikiwa kama Msemaji wa Familia  ninazo katika kiganja cha mikono yangu taarifa zote za umiliki wowote unaomgusa Lowassa.

Ninaweza kuuhakikishia umma kwamba yote aliyosema Waziri Kigwangala hayapo, na kama anayo basi sisi tuko tayari afanye lolote lililo chini ya mamlaka yake badala ya kurejea kule tulikopita ambako yeye na wenzake kadhaa walifanya bila mafanikio kuchafua heshima za wote anaowataja bila sababu .

Ni mimi
Fredrick Lowassa
Lowasa" Nimesikitishwa sana na Maneno ya Kigwangala" Lowasa" Nimesikitishwa sana na Maneno ya Kigwangala" Reviewed by KUSAGANEWS on January 29, 2018 Rating: 5

No comments: