Serikali imetakiwa kuongeza juhudi
katika kupambana na wafanyabiashara wanaoingiza na kutengeneza zana haramu za
Uvuvi badala ya kutumia nguvu nyingi kuziteketeza zana hizo kutoka kwa
wavuvi.
Akizungumza na wanachama wa umoja wa vijana we Chama Chama Mapinduzi (UVCCM)
mkoa wa Mara, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa, Kheri James amesema
umoja huo unaungana na serikali katika kupigwa vita uvuvi haramu lakini
unapingana na mbinu zinazotumika.
Amesema katika zoezi
linaloendelea hasa katika mikoa ya kanda ya ziwa badala ya kusaidia watumishi
wa serikali wanaotekeleza zoezi hilo wamekuwa wakichonganisha wananchi na
rais John Magufuli.
Juhudi zinazotumika katika kuchoma
zana hizo zinatakiwa kutumika kuhakikisha zana hizo haziingii nchini
kupitia mipaka yote na wala kutengenezwa na kuwepo katika masoko ya ndani ya
nchi,” alisema James</p></div><div><p>Amesema
Serikali inatakiwa kujiuliza ni kwani ni zana hizo haramu zimezagaa katika
soko la ndani na hatimaye kutumiwa na wavuvi wengi ambapo amesema kuwa
kukosekana kwa nyavu halali kunaweza kusababishwa na sababu nyingi ikiwemo
bei kubwa kutokana na ushuru wa nyavu hizo pamoja na malighafi zake kuwa juu.
Tusikubali operesheni chonganishi
ikiendeshwa kwa kisingizo cha kusimamia sheria, umemkamata mtu na nyavu
haramu ukazichoma, ukamtoza faini ya Sh20 milioni akalipa, bado unamchomea
mtumbwi wake na kumnyanga'nya samaki hivi huku ni kusimamia sheria au
kumkomoa mwanachi wa kawaida," amesisitiza mwenyekiti huyo
James amesema kuwa haiwezekani
serikali ikawaona watumiaji wa nyavu hizo na kushindwa kujua ni akina nani
wanaziingiza katika soko la Tanzania aidha kupitia mipakani au kutoka katika
viwanda vilivyopo nchini na kuzitaka mamlaka husika kuhakikisha kuwa wote
wanaojihusisha na biashara ya kutengeneza na kukuza zana hizo wanakamatwa na
kuchukuliwa hatua kali.
Amesema “iweleweke wazi kuwa sisi
UVCCM hautuungi mkono Uvuvi haramu ila tunapinga mbinu zinazotumika maana
zinalenga kumkomoa mnyonge sasa tunawataka wahusika waongeze juhudi
kuhakikisha kuwa wale wanaosababisha zana hizo kuwepo wanashughulikiwa kwa
mujibu wa sheria,”
Mmoja wa vijana wa chama hicho
wilayani hapaThomas John amesema vijana wengi wamekosa ajira na wengine
kuamua kujiajiri huku akiomba wapewe mitaji ili waweze kujiajiri vijana
wengi.
|
|
JITIHADA ZIONGEZWE KWENYE KUPAMBANA NA ZANA HARAMU.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment