Mahakama ya Mkoa wa Mwera imemuhukumu
mshtakiwa Simai Khamis Salum mwenye umri wa miaka 30 mkaazi wa Uzini wilaya ya
kati Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kutiwa hatiani kwakosa lakumuingilia
mwanamme mwenziwe kinyume na maumbile.
Imedaiwa Mahakamani hapo namuendesha
mashtaka Rahima Kheir mbele ya hakimu Muhammed Ali Muhammed kwamba mnamo tarehe
2/3 /2015 huko Uzini bila ya ridhaa kwamakusudi amefanya kitendo hicho
kwakijana mwenye umri wa miaka 20 jinalimehifadhiwa na kumsababishia maumivu
makali huku akijua jambo hilo ni kosa kisheria.
Akisoma hukumu Hakimu Muhammed
amesema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa kwa upande wa mashtaka na
kumuona nimkosa wakosa hilo ndipo Mahakama hiyo ilipomtia hatiani kutumikia
chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka saba pamoja na kumlipa fidia mtendewa yashilingi
Milioni mbili ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hiyo.
Ahukumiwa Kwa kumwingilia mwanaume kinyume cha maumbile
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment