Wanafamilia watano kati ya 10 wa Dar es salaam waliokuwa wakisafiri kwa Toyota Noah kwenda msibani Lyamungo, tarafa ya Machame, Kilimanjaro walifariki katika ajali ya gari iliyotokea Kabuku mkoani Tanga jana alfajiri.
Kati ya waliofariki wamo mtu na mkewe, huku mume huyo akiacha mke mdogo aliyebakia jijini Dar es salaam.
Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Kamishina msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe, ambaye alisema ajali hiyo ilitokea alfajiri ya jana ikihusisha gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T 893 DJQ iliyokuwa ikitoka Dar es salaam kwenda Moshi.
Alisema inahisiwa chanzo cha ajali ni dereva kupitiwa na usingizi kwa kuwa wasafiri hao waliondoka Dar es salaam usiku wa manane, na gari kuwa na abiria wengi kuliko uwezo wake. Kwa mujibu wa sheria Noah inatakiwa kubeba watu nane.
kamanda huyo aliwataja mke na mume waliofariki kuwa ni Bilal Marua (43) na Zainabu Marua (45), ambao ni wafanyabiashara wakazi wa Chamazi Magengeni.
Ndugu wengine waliofariki ni Neema Marua (54), Makame Muro (47) na Hidaya Idrisa (50), ambao wote maiti zao zilisafirishwa kwenda Moshi kwaajili ya mazishi jana, alisema.
Aliwataja majeruhi wa ajali kuwa ni Ayoub Marua ambaye alikuwa dereva, Maimuna Marua (46), Rashidi Idrisa (37), Madina Barahashi (49) na Arafa Idrisa, wote wafanyabiashara wakazi wa Chamazi na kwamba wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Alisema hadi sasa chanzo halisi cha ajali hakijafahamika, lakini gari liliacha njia na kuserereka porini.
“Ajali imetokea saa 11 alfajiri, muda huo walikuwa Kabuku. Maana yake waliondoka Dar es salaam usiku wa manane,” alisema Kamishna Bukombe.
“Kutoka Bukuku hadi Dar ni mwendo wa saa nne, kwa kuwa muda huo hakuna askari wa usalama barabarani inawezekana walikuwa wanatembea mwendo kasi.

Ajali yauwa familia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment