Wagombea nyadhifa mbali mbali wa shirikisho la miguu Tanzania TFF wameonywa na kutakiwa kufuata sheria za nchi na kukaa mbali na vitendo vya rushwa, kwa kipindi hiki ambacho wapo Dodoma kwa uchaguzi.
Akitoa onyo hilo Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Bwana Musa Chaulo, amesema TAKUKURU wapo macho kufuatilia kila hatua, na kwamba yeyote atakayekiuka sheria atachukuliwa hatua.
"Niwaombe tu Watanzania wote na viongozi wale wanaokuja kwenye uchaguzi, wajumbe wote waaokuja kwa ajili ya uchaguzi, wahakikishe kwamba wanafuata taratibu na sheria za nchi, yeyote ambaye atajihusisha na vitendo vya rushwa, vyombo vya dola vyote vipo tayari na vimejipanga, na tumejipanga tutashirikiana kuhakikisha kwamba wale wanaojihusisha na vitendo vya rushwa, wanadhibitiwa inavyopaswa", alisema Musa Chaulo
Viongozi na wajumbe mbali mbali wapo mkoani Dodoma kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu TFF, utakaofanyika hapo kesho tarehe 12 Agosti 2017.
No comments:
Post a Comment