Viongozi wa serikali wapigwa marufuku

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku viongozi wa serikali kufanya biashara ya pembejeo na vishada kama hawana mashamba ya tumbaku.

Waziri Majaliwa ametoa onyo hilo  wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku zaidi ya 600 wakiwemo wabunge, viongozi wa dini, chama na serikali kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isike-Mwanakiyungi, mjini Tabora.

"Kuna baadhi ya viongozi wa serikali hapa mkoani wamejiingiza kwenye biashara ya vishada na uuzaji wa pembejeo, hii ni dosari. Hatutaruhusu hili hata kidogo, Viongozi wa serikali ni lazima uwe shamba na ulime kisasa ili liwe ni shamba darasa kwa wakulima walio jirani nawe. Usifanye biashara ya pembejeo kama huna shamba," alisema Majaliwa.

Pamoja na hayo, Waziri Majaliwa amewataka viongozi wa AMCOS wasikubali kuuza vishada vya viongozi wa serikali kwani wakikamatwa watapelekwa jela.

Kwa upande mwingine, Waziri Majaliwa amesema endapo viongozi wa serikali wataamua kulima mashamba yao binafsi watalazimika kujiunga na vyama vya msingi (AMCOS) vya kwenye maeneo yao ili waweze kuuza kupitia huko kutokana na agizo la serikali linalokataza makampuni kununua tumbaku bila kupitia kwenye vyama vya msingi.

Viongozi wa serikali wapigwa marufuku Viongozi wa serikali wapigwa marufuku Reviewed by KUSAGANEWS on August 10, 2017 Rating: 5

No comments: