Watendaji wa vijiji vilivyopo wilayani Kibiti mkoani Pwani, wamezikimbia ofisi zao kwa hofu ya mauaji yaliyokatisha uhai wa takribani watu 40 katika miaka miwili, hivyo kusababisha shughuli mbalimbali za kijamii kukwama.
Taarifa hiyo iliyotolewa hapo jana na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Milongo Sanga, katika kikao cha robo mwaka cha baraza la madiwani, kilichokuwa kikijadili maendeleo ya wilaya hiyo ambapo aliwataka watendaji hao kurudi kuendelea na majukumu kutokana na ukweli kwamba hivi sasa hali ya usalama na amani imerejea.
Katika kikao hicho, kilichohudhuriwa na wakuu wa idara na madiwani, Katibu Tawala huyo aliwataka wananchi kuondoa hofu na kuendelee kufanya kazi zao kutokana na hali ya usalama kuimarika.
"Tunawaomba wenyeviti wa vijiji warudi kazini kuendelea na utoaji wa huduma kwa wananchi kwani usalama umeimarika na hakuna tena matatizo ya kiusalama" - alisema Sanga
No comments:
Post a Comment