Wakati leo ndiyo ilikuwa tarehe ya mwisho wa ulipaji
wa kodi za majengo ya mwaka 2016/2017, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imesogeza
mbele zoezi hilo hadi Julai 31.
Akizungumza Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema uamuzi huo umefikiwa
baada ya kuona bado kuna watu wengi wanahitaji kulipia kodi hiyo
Amesema kwa Jiji la Dar es Salaam zimetengwa ofisi maalumu
kwa ajili ya kazi hiyo hiyo ili kutoa fursa kwa ofisi nyingine kuendelea
kukusanya kodi nyingine
Kwa muda mrefu kidogo wahudumu wa TRA wamejikita zaidi
kwenye kodi ya majengo, sasa tumeona tutenge maeneo maalumu ili wanaolipa kodi
nyingine nao waendelee kuhudumiwa kwa ufanisi," amesema
Ofisi zitakazoendelea na zoezi hilo kwa Dar es Salaam ni TRA
Mbagala, Temeke, Kigamboni, Kimara, Tegeta, Manzese, Ilala, Gerezani,
Vingunguti, Samora, Kijitonyama na ofisi ya TRA ndani ya viwanja vya Sabasaba.
Kayombo amesema baada ya Julai 31 watakaolipa kodi hiyo
wataambatanisha na faini.
Muda ulipaji kodi ya majengo waongezwa hadi Julai 31
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 15, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment