Kontena hewa hewa la simu za I Phone 7 jana limemfikisha mahakamani, Mkurugenzi wa kampuni ya Candy& Candy, Josiah Kiman Kairuki(38), Mkazi wa Mikwecheni Jijini Dar es Salaam.
Kairuki ambaye ni Rais wa Kenya , anatuhumiwa kujipatia kiasi cha sh 336 milioni kwa udanganyifu kutoka kwa Yusuph Mohamed ili akombowe kontena hilo katika bandari ya Dar es Salaam, kitu ambacho ni uongo.
Mwendesha mashitaka wa polisi,Anzelini Muhela, alieleza mahakamani, mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Longido,Aziza Temu kuwa mtuhumiwa huyo amejipatia fedha hizo kati ya Januari 23 na june 10, 2017.
Mwendesha mashitaka alisema upelelezi wa shauri hilo, haujakamilika na aliomba mtuhumiwa huyo asipewe dhamana kwani,uraia wake una utata akiwa nje anaweza kusababisha kupotea kwa nyaraka za kesi na kiasi alichojipatia ni kikubwa na akiwa dhamana anaweza kutoweka.
Hata hivyo, Wakili wa Kairuki, John Mallya alipinga hoja zote za mwendesha mashitaka na kueleza dhamana ni haki ya kikatiba ya mtuhumiwa ambaye bado hajatia hatiani.
Mallya alisema pia maombi hayo ya jamuhuri, yalitakiwa kuwasilishwa chini ya kiapo kwa mujibu wa mwenendo wa makosa ya jinai sura 396(A) kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2011.
Hakimu Temu aliahirisha kesi hiyo, hadi julai 26 mwaka huu, ambapo atatoa maamuzi ya kumpa dhamana mtuhumiwa huyo ama kutompa.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 21, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment