Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Dk. Wilson Mahera anawatangazia wananchi wote kuhudhuria kwenye MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI utakaofanyika Jumatatu tarehe 17.07.2017 kwenye Ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha eneo la Sekei kuanzia saa 03:30 asubuhi.
Mkutano huo ni wa kujadili taarifa za robo ya nne kuanzia Aprili mpaka Juni, 2017 Mkutano huu uakuwa ni mkutano wa mwisho kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Mkutano utakuwa na agenda 12 agenda kuu ikiwa ni pamoja na:-
1. MASWALI YA PAPO KWA PAPO
2. TAARIFAFA YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWEZI JUNI
3. TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MIEZI MITATU
4. TAARIFA YA MREJESHO WA BAJETI YA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2017/2018
5. MAPENDEKEZO YA KUANZISHA WILAYA MPYA KUTOKA WILAYA YA ARUMERU
6. KUPOKEA MIHTASARI YA KAMATI 4 ZA KUDUMU ZA HALMASHAURI
Mkutano huu ni mkutano wa wazi hivyo wananchi wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa ili kufahamu maendeleo, changamoto na mikakati ya halmashauri katika kufikia malengo.
FIKA BILA KUKOSA KWA MAENDELEO YA HALMASHAURI YETU YA ARUSHA
No comments:
Post a Comment