BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA ARUSHA LIMEPOKEA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI MWEZI MACHI 2017.

Baraza la Madiwani halmashauri ya Arusha limejadili  na kupokea taarifa ya mapato na matumizi kwa mwezi machi  2017.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo robo ya nne kipindi cha mwezi aprili hadi juni 30 katika baraza la madiwani mweka hazina wa halmashauri ya Arusha Innocent Mariki amesema mwezi machi halmashauri ilikusanya kiasi cha shilingi b 2.9 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali.

Bwana Mariki amesema makisio ni shilingi bilioni  3.2 ambayo ni sawa na asilimia 65.17 na kufikia mwezi machi halmashauri ilipokea shilingi bilioni  25.9 ya mishahara na matumizi mengineyo ya shilingi bilioni  36 sawa na asilimia 71.02.

Kwa upande wa matumizi kwa mwezi machi  2017 halmashauri hiyo imetumia shilingi bilioni  2.19 na maeneo yasiyo na ruzuku ni asilimia 62.88

Baada ya tarifa hiyo kuwasilishwa Baraza hilo wepokea na kujadili na kuridhia.

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA ARUSHA LIMEPOKEA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI MWEZI MACHI 2017. BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA ARUSHA LIMEPOKEA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI MWEZI MACHI 2017. Reviewed by KUSAGANEWS on July 17, 2017 Rating: 5

No comments: