Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo akifungua Kikao cha kwanza cha Kamati ya Amani ya viongozi
wa dini Mkoa kilichofanyika Ofisini.
|
| Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Arusha Bi. Jacquline Kapila akielezea kazi za Taasisi yake kwa viongozi wa Dini kwenye kikao cha kamati ya Amani. |
|
Sheikh Mkuu
wa Bakwata mkoa wa Arusha, Shabaan Juma
akichangia kwenye Kikao cha Kamati y Amani kwa kawataka wananchi kudumisha
amani na kujenga utamaduni wa kuvumiliana.
|
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo akiongea na viongozi wa Dini wakati wa Kikao cha Kamati ya Amani |
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo(katikati) katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Dini
waliohudhuria Kikao cha Kamati ya Amani.
|
Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA)
Mkoani Arusha Ndg. Apili Mbaruku akijibu hoja za viongozi
wa dini wakati wa Kikao cha Kamati
ya Amani.
|
|
Sheikh Mkuu
wa Bakwata mkoa wa Arusha, Shabaan Juma
akichangia kwenye Kikao cha Kamati y Amani kwa kawataka wananchi kudumisha
amani na kujenga utamaduni wa kuvumiliana.
|
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mhe Mrisho Mashaka Gambo amekutana na kamati ya Amani ya Mkoa
ambayo inajumuisha viongozi wa dini mbalimbali zilizoko katoka Mkoa huu kuzungumzia
mustakabali wa Amani na namna viongozi hawa wa dini
watashirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo kwa
wananchi ambao ni waumini wao.
Akizungumza katika
Kikao hicho Mhe. Gambo alisema kazi
ya Ulinzi wa Amani itakua rahisi sana kupitia viongozi wa dini ambao wana
karama ya kuongea na kubadilisha maisha ya watu bila kutumia nguvu ama
kuwashurutisha isipokua kwa chakula cha roho ambacho hujenga misingi
imara ya imani na tabia njema.
Maendeleo ya wananchi
hayawezi kupatikana bila Amani kuwepo katika Mkoa wetu ni lazima tusaidiane
katika hili dhamira yetu ifanikiwe kwa wepesi zaidi tuna Imani kubwa sana Na
viongozi wetu wa dini na ndio maana nikaona ni vyema tukakutana ili tusikie
kutoka kwenu ninyi ambao mnawakilisha kundi kubwa la wananchi na pia
kufahamu kero mbalimbali zinazowakwaza wananchi katika maeneo yenu
alisema Gambo.
Askofu wa Dayosisi ya
Kaskazini Kati KKKT Solomon Masangwa akichangia kuhusu
masuala yanayoweza kuhatarisha amani alisema kundi ambalo linatakiwa
kuangaliwa kwa jicho la Tatu na litasaidia sana katika ulinzi wa Amani ni
waendesha boda boda pamoja na wanachinga ambao kwa sasa wanaonekana kutopewa
kipaumbele au hatuwajali kwa kiasi kinachostahili.
Tunapaswa kuangalia namna
gani watu wanaofanya shughuli hizi wanakua rasmi kwa kupatiwa maeneo maalumu
pamoja na utambulisho utakaowawezesha kufanya kazi zao kwa Amani na kujipatia
kipato cha kuendesha maisha yao na si kama walivyo sasa wanafanya kazi hizo
katika maeneo yasiyo rasmi na kuhama kila siku hali hii ina wafanya wajihisi
kama si sehemu ya Taifa hili hivyo wanaweza kutumika kiurahisi kuhatarisha
amani ya Nchi yetu alisema Masangwa.
Akichangia katika
viashiria vya uvunjifu wa amani Askofu Dr. Leornard
Mwizarubi wa Kanisa la SAYUNI EAG
(T) alisema ni vyema Serikali ikajikita katika kutatua changamoto
zinazoathiri maisha ya kila siku ya wananchi ili hata sisi viongozi wa dini tunapoongea na waumini tuwe na vielelezo
dhabiti vya kuonyesha namna ambavyo Serikali kero zao zimeshughulikiwa.
Aliendelea
kusema “Katika eneo ambalo ninatoa huduma ya Kiroho kwenye Kata za Unga Ltd,
Sokoni 1, Daraja II, Sinoni na maeneo ya jirani wakazi wa mitaa hiyo wanapata
shida sana ya huduma ya maji Taka na hata katika Kanisa langu inanilazimu
kutafuta gari la kunyonya maji taka mara tatu kwa wiki ili kufanya mazingira
kuwa safi, sasa kuna maeneo mengine wananchi hao hawana uwezo wa kutafuta gari
hilo la kunyonya maji taka hivyo wanaishia kulalamika kwa kuishi katika
mazingira machafu”.
Aidha Sheikh Mkuu wa Bakwata mkoa wa Arusha, Shabaan Juma alishkuru Sekretariet ya Mkoa kwa kikao hiki muhimu
kwa ustawi wa jamii ya Arusha na kueleza kuwa katika kipindi hiki cha Mpito
Nchi yetu inahitaji maombi ya bila kikomo ili kuweza kuvuka salama na
tunategemea kuendelea kuona mabadiliko katika kila eneo; Tunaamini si wote wanafurahia mabadiliko haya hivyo tuna wajibu
wa kuwajulisha waumini wetu kuhusu umuhimu wa mabadiliko ya mifumo katika
uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano na faida zitakazo patikana kwa Taifa.
Akiwasilisha changamoto katika upande wake Sheikh Shaaban alisema
“Kuna ukuaji wa kasi ya makazi holela katika Jiji la Arusha, Utaratibu wa mipango miji hauzingatiwi na hii
inasabisha maeneo mengi kutopitika kwa urahisi hivyo hata itakapotokea dharua
sio tahisi kwa wananchi wetu kupata msaada wa haraka, tunaomba wanachi wapimiwe
maeneo yao, barabara zifunguliwe ili huduma muhimu ziweze kufika katika maeneo
hayo”.
Mkurugenzi wa Idara ya maji safi na maji Taka (AUWASA) Eng. Ruth
Koya alisema Taasisi yake inaanza utekelezaji wa Mradi mkubwa wa maji safi na
Taka ambao matatizo yote yaliyowasilishwa katika kikao hiki yanayohusiana na
maji yatashughuliwa kupitia mradi huo.
Aliongeza kuwa mradi huo utahusisha uboreshaji wa mioundombinu ya
maji safi, Uhamishaji wa mabwawa ya maji Taka(yaliyokuwa Lemara kwa hivi sasa),
ununuzi wa magari ya kunyonyea maji machafu pamoja na magari ya kusambaza na
kuuza maji safi.
Mkuu wa Mkoa Mge. Gambo alitolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali
zilizowasilishwa na kuelezea namna ambavyo Changamoto ya Mipango Miji
ilivyopata ufumbuzi kupitia ukamilishaji wa
Mpango Mkakati wa Jiji la Arusha (Master Plan) na kuwajulisha wajumbe
kuwa mpango umekamilisha na umekwishapitiwa na Halmashauri zote tatu
zinazohusika, hivyo kwa hivi sasa utawasilishwa Wizarani na taratibu zote
zikikamilika utekelezaji utaanza mara moja.
Kuhusu suala la Machinga na waendesha boda boda boda Rc Gambo
alisema Serikali imekwisha anza utaratibu wa kutafuta maeneo salama na
rafiki kwa ajili ya wafanyabishara
ndogondogo maarufu kama machinga na tutaongea nao ili tuwe na makubalino ya
pamoja.
Aidha kuhusu bodabdoa tumeanza kuwatambua kupitia kwenye uongozi
wa mitaa na vituo vyao na tutahakikisha tunaboresha mazingira yoa ya kufanyia
kazi na zaidi tunawatafutia Pikipiki ambazo
watapewa Vijana wanaofanya biashara ya boda boda kwa utaratibu maalumu;
Itawapasa kurudisha Fedha za Pikipiki tu na kisha kupata umiliki halali ya
Chombo hicho tofauti na sasa hivi ambapo wanapewa pikipiki hizo na kulipa mara
mbili ya bei kwa matajiri wao ndipo wapate Umiliki alimalizia Gambo.
RC GAMBO AONGOZA KIKAO CHA KWANZA CHA KAMATI YA AMANI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 13, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment