|
Wananchi wa
Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya
Ngorongoro wakishangilia Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ulipokuwa unawasili
katika Kijiji hicho.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(Mbele kushoto) pamoja na
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo(Mbele Kulia) wakiwasili kwenye Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Esokonoi.
|
|
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Arusha Mhe. Michael Lekule Laizer
akiongea na wananchi wa Kijiji cha Esokonoi wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa
katika Wilaya hiyo.
|
|
Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi wakimskilizia Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mhe. Mrisho Gambo (hayupo
pichani) alipokua akizungumza nao kwenye Mkutano wa hadhara.
|
|
Watoto wa Jamii ya Kimasaai pia walihudhuria Mkutano wakati wa
Ziara ya Mkuu wa Mkoa w Arusha katika Wilaya ya Longido.
|
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Juma
Mhina ameamuru polisi wa Wilaya hiyo kumkamata na kumuweka ndani Mtendaji wa Kata ya Gilai Lumbwa, Paul Lucas
baada ya kutuhumiwa kutumia Fedha za umma vibaya zilizochangwa na wananchi wa
maeneo hayo kwa ajili ya kuinua Sekta ya Elimu.
Agizo hilo la Mhina lilifanikiwa baada ya mara kwa mara
kushindwa kumkamata Paulo baada ya kumkwepa kila alipokuwa akitafutwa na
hatimaye mtendaji huyo kujitokeza kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mhe Mrisgo Gambo uliofanyika kwenye Kijiji cha IIchang Sapukin kata ya
Gilailumbwa.
Mmoja kati ya wananchi walioshirki Mkutano huo Bi. Anni
Mollel alimshukuru Rc Gambo kufika Kijijini hapo na kujionea hali halisi ya
ujenzi wa Shule ya Sekondari ambayo wananchi walichanga Fedha zao zaidi ya Tsh
Mil 96 ila hazikutumika kama ilivyokusudiwa badala yake viongozi wa Serikali na
Wenyeviti wa Kijiji walitumia Fedha hizo kujinufaisha binafsi badala ya
kuwasaidia watoto kukaa kwenye mazingira mazuri ili wapate Elimu.
“Yaan bora umekuja Mkuu hawa viongozi wetu huku kijijini
ni Miungu watu wanajipangia mambo yao ya kubadilisha matumizi ya Fedha zilizochangwa na wananchi kaka zao yaan
ukiwaangalia wao wana maisha mazuri wakati sisi tunateseka sasa lro uondoke nao
na tunamuomba Mkurugenzi wa Halmashauri hii Ndg. Mhina kuwaleta watumishi
wengine na wale waliohamishwa hapa baada ya kushirki kula hela zetu wakamatwe
pia na waseme wamepeleka wapi hela zetu”
Mara baada ya wananchi kusema hayo Gambo alimhoji
Mkurugenzi Mhina ni kwa nini hawajachukua hatua za kisheria kuwakamata watuhumiwa ndipo Mhina
aliposema mbele ya hadhara hiyo kwamba
zoezi hilo lilishindikana awali baada ya Paulo kumkwepa Mkurugenzi huyo mara
kwa mara lakini jana alijileta mwenyewe katika mkutano huo na ndipo imekuwa rahisi kwake kumkamata.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkaguzi wa ndani wa
Halmahauri hiyo, Bi. Mwajuma Mndaira kwenye
Mkutano huo alidai kuwa alifanya mahojiano na wenyeviti wa vijiji kujua
ni kwa nini walikusanya Fedha kwa wananchi bila kutumia stakabadhi za Serikali
katika zoezi hilo.
Pia hivi sasa bado wananendelea na uchunguzi wa nyaraka
za malalamiko mbalimbali ili kubaini Paulo alihusika na kinanani na kwa nini
abadilishe baadhi ya matumizi ya Fedha hizo na kuuza baadhi ya vitu vilivyochangwa bila kuonyesha
sababu ya Msingi kwani baadhi ya kampuni za uwindaji wa kitalii ikiwemo Wingert
WindroseSafaris na Kampuni ya Kilombero Nothern Safaris zilitoa mifuko ya
Saruji 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari hiyo.
Rc Gambo alimuhoji Mtendaji huyo kwanini shule hiyo
haijakamilika mpaka leo wakati watoto wa jamii ya kifugaji wana haki ya
Kupata Elimu na wazazi wao wanajitoa wa ajili ya watoto wao huku yeye
akiendelea kuwarudisha nyuma, Paulo alijitetea kwamba baadhi ya fedha hizo
ziliztumika kihalali na fedha zingine alilazimik kubadilisha matumizi yake na
kujenga vyumba vya maabara, jiko pamoja na mabweni,
Baada ya utetezi wake kugonga mwamba alijikuta yupo
chini ya himaya ya Polisi waliokuwa wakiongoza msafara huo ambapo pia Mkuu wa
Wilaya hiyo Chongolo aliahidi wananchi hao kuwa atafuatilia suala la
watumishi wengine watakoziba nafasi za
wote watakaomatwa na ubadhirifu huu kuletwa haraka iwezekanavyo ili huduma
zisizorote na endapo tuhuma hizi zikithibitkka watapelekwa Mahakamani na aliongezwa kuwa atakua karibu nao
kuhakikisha kero kama hizo hazijitokezi rena hapo baadae .
Mtendaji wa Kata aswekwa Rumande kwa Matumizi mabaya ya Fedha za Umma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 27, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment