Watu 11 wamefariki dunia papohapo na wengine 46 kujeruhiwa katika
ajali mbaya iliyotokea eneo la Veta Dakawa barabara ya Morogoro Dodoma
kwa kuhusisha magari matatu,kufuatia roli la mafuta kugongana uso kwa
uso na gari la mizigo na kisha kuwaka moto majira ya saa 12 jioni na
badaye basi la kampuni ya Ota Expresi likitokea Bukoba kuelekea Dar es
Salaam kuyagonga magari hayo na kusababisha vifo vya watu sita.
Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro
Ulrich Matei aliyefika eneo ka tukio zimesema ajali yà kwanza ilihusisha
gari ndogo aina ya Noah ambayo haijakutwa eneo la tukio ambayo ilikuwa
ikijaribu kulipita Lori lililokuwa limebeba kontena lenye mchele Na
vitunguu likitokea uelekeo wa Dodoma kuelekea Morogoro.
Akabainisha kuwa Noah mbele ikakutana Na Lori la mafuta (tanker)
ambalo katika kujaribu kuikwepa Noah ikakutana uso kwa uso na Lori
lililokuwa likikokota kontena lenye mchele Na Magari hayo kuwaka moto Na
kupinduka.
Amesema katika ajali hiyo,wà tu watano wamepoteza maisha wakiwemo
wanawake wawili waliokuwa abiria ndani Ya Lori lenye kontena, Na Mtu
mwingine mmoja pamoja Na maiti nyingine tatu ambazo hazikutambuliwa ni
za kina Nani baada ya kuungua vibaya.
Kamanda Matei amesema wakati jitihada za Askari polisi kwa
kushirikiana na kikosi cha zimamoto wakiendelea na shughuli za uokoaji
eneo la ajali hiyo iliyotokea kuanzia Juni 30,majira ya saa 11 jioni,
ilipofika Julà i Mosi majira ya saa 10 alfajiri ilitokea ajali Nyingine
iliyohusisha basi la abiria.
Amesema ajali hiyo ilihusisha basi la abiria Mali ya kampuni ya Ota
High Class yenye namba za usaliji T 201 DGK iliyokuwa ikitokea Bukoba
kuelekea Jijini Dar es salaam ambayo kutokana Na mwendo kasi dereva wake
alishindwa kumudu Na kuligonga Lori la mafuta lililopata ajali YA awali
Na kupinduka.
Katika ajali hiyo iliyohusisha basi,wà tu sita wamepoteza maisha
papo Hapo Na wengine ambao idadii yao hakijaweza kujulikana Mara moja
walijeruhuwa nna kukimbizwa hospitali ya Rufaa YA Mkoa wa Morogoro Na
kituo cha Afya Dumla kwa matibabu.
Mmoja wa mashuhuda waliokutwa eneo la Tukio,Japhet Suleiman,mkà zi
wa Dakawa ambaye ni mwendesha pikipiki za abiria katika eneo
hilo,anasema alikuwa Na wenzake,wakiwa watatu,walitoka kuwapokea abiria
waliokuwa kwenye Noah na wakastukia mahindi Mkubwa ulioambatana Na
moto,ambapo mwenzao mmoja anayejulikana maarufu kwa jina la Simba
alishindwa kujiokoa na kupoteza maisha hukummwingine akijeruhiwa usoni.
Aidha Sultan Hamis Suleiman amesema alipata taarifa za ajali ya
gari ya Mjomba wake,ambayo ndio ilitokea Na mchele ikitokea Mtukula
kuelekea jijini Dar,ambapo alikiri vifo vya abiria wanawake wawili na
mtu mwingine mmoja ambayo hajamtambua bado,Katika gari hiyo,huku
msmamizi wa gari hiyo Said Saum Said akinusurika na amepelekwa Jijini
Dar es salaam kwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya.
Mwandishi wa Habari hizi ameshuhudia Magari yaliyohusika nà ajali
katika eneo la tukio,ambapo lori lililokuwa na mchele likiendelea kufuka
Moshi kutokana ña Bidhaa zilizokuwemo kuungua Sambamba na Lori, basi la
Ota lililokuwa limesogezwa pembeni ya barabara kupisha Magari kupita
barabara kuu ya Morogoro Dodoma kukiwa limefutwa kabisa palipokwa na
jina kwa kutumià kemikali,mabaki ya kichwa cha tanker na pikipiki tatu
zilizoungua kabisa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Stephen Kebwe ambaye naye amefika
eneo la tukio,amelaani vikali kitendo Madereva wanaoendesha bila
kufuata Sheria,kanuni Na taratibu za usalama barabarani,na kuwataka
wananchi kukaa Mbali Na eneo la ajalli Na wasijaribu kuchota mafuta
kwani eneo hilo sio salama,Sambamba na polisi kulinda usalama wa
wananchi Na mali zao Na kuweka vizuizi kuepusha athari zaidi kujitokeza.
Kebwe pia amewaagiza wakala wa barabara Tanroads Mkoa wa Morogoro
kumwaga mchanga katika eneo la ajali kudhibiti utelezi wa mafuta
yaliyomwagika kwenye lami ili utelezi uliopo usisababishe ajali Nyingine
zaidi.
Watu 11 wamefariki,46 kujeruhiwa katika ajali Morogoro.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 01, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 01, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment