MTU MMOJA AKAMATWA KWA KUMKATA MATITI MWANAMKE KILIMANJARO

kamanda wa polisi mkoa wa kilimanjaro Wilbroad Mtafungwa


Polisi mkoani Kilimanjaro, imetia mbaroni mtu anaedaiwa kumkata mwanamke mmoja mkazi wa chekereni, maziwa yote mawili, baada ya kukataa kufanya nae mapenzi.

Akidhibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa, amesema mtuhumiwa huyo anayefahamika kwa jina la  Arnold Josephat, amekamatwa jana Juni 29 mwaka huu,majira ya usiku, baada ya jeshi hilo kupata taarifa kwa raia wema,kuwa mtuhumiwa huyo ameingia kwa siri, kijiji hapo.

Kamanda amesema tukio la kukatwa matiti kwa mwanamke huyo  aitwae Mary Aloyce Lyimo, (23), mkazi wa Chekereni, wilaya ya Moshi, lilitokea Februari 7, mwaka huu,ambapo mtuhumiwa baada ya kufanya tukio hilo alikimbia.

Akielezea mazingira ya tukio hilo, Kamanda amesema siku ya tukio, kijana huyo alimtokea mwanamama huyo nyumbani kwake,huku akiwa ameshika panga mkononi na kutaka kufanya nae mapenzi kwa lazima, lakini alipokataa ndipo alipomvua nguo kwa nguvu, na kumkata maziwa yote mawili, kisha  kuyaweka kwenye mfuko wa malboro na kuondoka nayo.

Amesema  Juni 29, mwaka huu  usiku, polisi walipata taarifa ya kuwa mtuhumiwa huyo ameonekana maeneo ya kijijini hapo na ndipo wapeleleziwalipokwenda na kufanikiwa kumtia mbaroni.

Aidha amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa  huyo,kutasaidia kuimarisha uchunguzi wa jeshi hilo ambao ulikuwa unaendelea tangu kutokea kwa tukio hilo, na kwamba baada uchunguzi huo, mtuhimiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.


Katika tukio lingine,jeshi la polisi mkaoni Kilimanjaro, linafanya
uchunguzi kuhusiana na tukio la wasichana wawili kukeketwa, wakati tayari serikali ilishapiga marufuku  vitendo hivyo viovu.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Wilbroad Mutafungwa, amesema wasichana hao ambao  majina yao yanahifadhiwa kutokana na umri wao kuwa mdogo, waligundulika kufanyiwa vitendo hivyo baada ya  walimu wao kuwaona wakitembea isivyokawaida.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi,juni 22 mwaka huu,
wasichana hao wanaoishi kijiji cha Sanya Stesheni, wilayani Hai,
walichukuliwa shuleni wanakosama, ambapo ni shule ya Msingi Obran, na Baba yao mkubwa kwa kuomba ruhusa kuwa wanakwenda kwenye Ubarikio.

Amesema baada ya kuchukuliwa na baba yao mkubwa, walipelekwa kijiji cha Lengasiti Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, na  kesho yake, wakiwa kijijini humo, wanawake wawili walifika na kuwachukua kwa nguvu na hatimae kuwakeketa.

Kamanda amesema baada ya tukio hilo, walirudi shuleni wakiwa katika hali hiyo hadi pale walimu wao walipoigundua hali yao, na kutoa taarifa hiyo polisi.


Aidha amesema kwa kuwa tukio hilo lilitokea eneo la Lengasiti, wilaya Simanjiro, jeshi la polisi mkoani humo linaanda jalada na kulipeleka mkoani Manyara kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
MTU MMOJA AKAMATWA KWA KUMKATA MATITI MWANAMKE KILIMANJARO MTU MMOJA AKAMATWA KWA KUMKATA MATITI MWANAMKE KILIMANJARO Reviewed by KUSAGANEWS on June 30, 2016 Rating: 5

No comments: