Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia Mchungaji wa
Kanisa la Victory lililopo Sokoni One CHRISANTUS MBOYA kwa tuhuma za kumbaka
msichana mwenye umri wa miaka 17 aliye na matatizo ya kiafya kwa muda mrefu ambaye
anaishi na Dada yake eneo la Moshono mkoani hapa.
Akizungumza na vyombo vya habari Kwa niaba ya kamanda wa polisi Kaimu Kamanda wa Polisi
mkoani Arusha Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Yusuph Ilembo amesema
tukio hilo June 3 mwaka huu saa nne asubuhi katika eneo la Sokoni One nyumbani
kwa mchungaji huyo wakati mke wake akiwa hayupo.
Amesema Msichana huyo ni muumini katika Kanisa hilo na
kutokana na hali yake ya afya mchungaji huyo aliitumia fursa hiyo kumwita
kwenda nyumbani kwake ili akamfanyie maombi kwa madai kwamba alikuwa amelishwa
sumu na wachawi na alipokwenda badala ya kumfanyia maombi alimbaka.
Amesema baada ya kitendo hicho mchungaji huyo alimwambia
asimwambie mtu yeyote; ambapo June 10 majira ya saa tano asubuhi dada yake
alichukua simu ya msichana huyo na kuuona ujumbe uliotoka kwenye simu ya
mchungaji huyo wa kumwomba radhi kwa kitendo kilichofanyika.
Kamanda Ilembo ameongeza kuwa baada ya msichana huyo
kuhojiwa alieleza yote yaliyotokea na ndipo taarifa zikapelekwa katika kituo
kikuu cha polisi Arusha kwa hatua zaidi;na kwamba kutokana na afya ya msichana
huyo alipewa PF3 na kwenda hospitali ya Mount-Meru ambako amelazwa kwa
uchunguzi zaidi.
MCHUNGAJI WA KANISA AMBAKA MTOTO WA MIAKA 17 ARUSHA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 12, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 12, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment