Baada ya
kuhangaika kwa muda mrefu, hatimaye Simba wamefanikiwa kuongoza Ligi Kuu
Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya jana kuichapa Stand United kwa bao
2-1 mchezo uliopigwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga. Bao la Simba lililowafanya
wakae kileleni liliwekwa kimiani na Hamis Kiiza dakika ya 34, baada ya kupata
pande safi kutoka kwa Ramadhan Kessy.
Hii ilitokana na Simba kugongeana pasi safi,
kabla ya kumkuta Kessy aliyemimina krosi maridadi kwa Kiiza aliyemchungulia
golikipa Frank Muwonge na kumtungua. Dakika ya 51, Kiiza kwa mara nyingine
aliifungia Simba bao la pili kutokana na juhudi zake binafsi. Hilo linakuwa bao
la 16 kwa Kiiza, ambaye sasa ndiye anayeongoza kwa mabao akifuatiwa na Amisi
Tambwe wa Yanga aliye na mabao 14.
Ushindi huo, umeifanya pia Simba ikae
kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 45, wakifuatiwa na Yanga walio
na pointi 43, huku Azam ikiwa na pointi 44. Azam wanaweza kusogea nafasi ya
pili kama watashinda katika mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa
kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mchezo huo ulikuwa na kosakosa kadhaa,
lakini nafasi ambazo Simba watazijutia ni ile ya dakika ya 49, pale Ibrahim
Hajib aliposhindwa kufunga akiwa amebaki na lango.
Kiiza pia alipoteza nafasi nzuri ya kufunga
dakika ya 37, baada ya kupewa pasi safi na Said Ndemla na kushindwa kulenga
lango. Stand United: Frank Muwonge, Revocatus Richard, Seleman Mrisho, Nassor
Masoud, David Osman, Jacob Massawe, Pastory Athanas, Amri Kiemba, Elius Maguli,
Seleman Salembe, Vitalis Mayanga. Simba: Vicent Angaban, Hassan Kessy, Emery
Nimubona, Abdi Banda, Juuko Murshid, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas
Mkude, Hamis Kiiza, Ibrahim Ajib, Said Ndemla.
Simba yakaa kileleni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 14, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 14, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment