KIFO CHA PAPA WEMBA CHAHARIBU MIPANGO YA DIAMOND

Kwenye ukurasa wake wa Facebook Diamond ameelezea huzuni hiyo, huku akitoa taarifa kuwa kulikuwa na mipango mingi ya wao kufanya kazi, lakini mauti yameshafuta mipango hiyo.

“Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halafu ghafla naskia habari ya msiba...Dah! nimesikitika sana. Hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyez Mungu ndiyo mpangaji...Pumzika salama Kiongozi wetu daima tutakukumbuka” aliandika Diamond Plutnums kwenye ukurasa wake wa facebook

Msanii Papa Wemba amefariki dunia jana baada ya kuanguka akiwa jukwaani akiimba na kufariki papo hapo nchi Ivory Coast.
KIFO CHA PAPA WEMBA CHAHARIBU MIPANGO YA DIAMOND KIFO CHA PAPA WEMBA CHAHARIBU MIPANGO YA DIAMOND Reviewed by KUSAGANEWS on April 28, 2016 Rating: 5

No comments: